Story by Our Correspondents-
Bunge la Seneti alasiri ya leo litakuwa na kikao maalum cha kujadili hoja ya kubanduliwa mamlakani kwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza iliyowasilishwa mbele ya bunge hilo na wawakilishi wadi wa kaunti ya Meru wiki iliyopita.
Spika wa bunge la Seneti Amason Jefwa Kingi amesema kikao hicho ni cha dharura ikizingatiwa kwamba bunge liko katika likizo lakini kutokana na uzito wa hoja hiyo imelizalizimu bunge kuijadili.
Spika Kingi amesema tayari Kiongozi wa walio wengi katika bunge la Seneti Aaron Cheruiyot na Spika wa bunge la kaunti ya Meru Ayub Bundi wamechapisha
nakala ya hoja hiyo katika gazeti rasmi la serikali baada ya kukamilisha ripoti ya kubanduliwa mamlakani Gavana Kawira.
Maswala yanayomuandama Gavana Kawira ni pamoja na utumizi mbaya wa afisi ya umma, kutumia mamlaka yake vibaya na kufanya uteuzi wa viongozi kwa kukosa kuzingatia kanuni na sheria.