Picha kwa hisani
Bunge la kaunti ya Kwale limeteuwa Kamati maalum ya wajumbe 7 kuchunguza barua ya ombi lililowasilisha na Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya la kutaka kupewa mda zaidi kabla ya kufika mbele ya bunge hilo.
Mvurya alikuwa ameagizwa kufika mbele ya bunge hilo hii leo ili kueleza sintofahamu iliopo kati ya bunge hilo na serikali ya kaunti baada ya mzozo kuibuka kuhusu matumizi ya fedha na bajeti ya zaidi ya shilingi milioni 160 iliopitishwa na bungeni hilo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya vikao vya bunge, Spika wa bunge hilo Sammy Ruwa amesema wajumbe hao 7, watachunguza vigezo vilivyoidhinishwa ndani ya barua hiyo na kuwasilisha ripoti bungeni ambao itapelekea siku maalam ya Gavana huyo kufika mbele ya bunge hilo.
Kwa upande wake Kiongozi wa wachache katika bunge hilo Ndoro Mwaruphe amesema sio makosa kwa Gavana huyo kufika mbele ya bunge hilo kutoa taarifa kuhusu shughuli za serikali ya kaunti hiyo.