Picha kwa hisani –
Kumezuka mdahalo mkali katika bunge la kitaifa, wakati wa kujadili kauli iliotolewa na Jaji mkuu nchini David Maraga ya kumshinikiza Rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge kwa kukosa kuupitishwa mswada wa thuluthi mbili ya usawa wa jinsia.
Kiongozi wa wachache bungeni humo John Mbadi amesema Jaji Maraga hana mamlaka ya kumshauri Rais Kenyetta kulivunja bunge huku akisema mswada huo unafaa kusuluhishwa kupitia refurendem.
Akitetea hoja hiyo bungeni, Mbunge wa Mbita Millie Odhiambo, amesema ni lazima wabunge waungane na kuutathmini mswada huo ili wanawake wajumishwe kikamilifu katika nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini.
Hata hivyo kauli ya Millie imepingwa vikali na Kiranja wa wachache bungeni, Chris Wamalwa, aliyesema mswada huo uliwasilishwa mara kadhaa bungeni na idadi ya wabunge wakike walikwepa vikao hivyo kwa maslahi yao binafsi.