Picha kwa hisani –
Bunge la kaunti ya Kirinyaga limefungwa kwa muda wa wiki mbili, baada ya wabunge na wafanyazi kuambukizwa virusi vya corona.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, spika wa bunge hilo Anthony Gathumbi, amesema kufungwa kwa bunge hilo kutatoa nafasi ya kunyunyiziwa dawa na kuendelea kuzingatia kanuni za wizara ya afya za kukabiliana na covid-19, sawai na kuruhusu kujitenga kwa wale walioambukizwa virusi hivyo.
Gathumbi aidha amewarai wajumbe kuzingatia kanuni zote zilizowekwa dhidi ya virusi vya corona.
Huku hayo yakijiri mwakilishi wa wadi ya London katika bunge la kaunti ya Nakuru samwel karanja, ameaga dunia baada ya kugua kwa mda mfupi.
Gavana wa Nakuru Lee Kinyajui, amethibitisha kifo cha mjumbe huyo mapema leo, ikiwa ni wiki mbili tu baada ya mwakilishi wa wadi ya Hells Gate John Njuguna kurafiki kufuatia virusi hivyo vya corona.