Bunge la Kaunti ya Taita Taveta linaomboleza kifo cha mmoja wao Bi Anastancia Wakesho Mombo.
Mjumbe huyo maalum amekuwa akiugua kwa muda tangu kuteuliwa kwake katika bunge la Kaunti hiyo ana ameaga dunia mapema leo.
Gavana wa Kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amedhihirisha masikitiko yake na kuihakikishia familia ya marehemu Wakesho msaada kwao wakati huu bunge hilo linapozidi kuomboleza kifo chake.
Samboja amemtaja Bi Wakesho kama Kiongozi muadilifu na aliyejizatiti kuyatekeleza barabara majukumu yake licha ya kuugua.