Story Bakari Ali:
Bunge la kaunti ya Mombasa limerejelea rasmi vikao vyake baada ya likizo ndefu huku miswada muhimu ikipewa kipau mbele kujadiliwa katika bunge hilo ili kuwanufaisha wakaazi wa Mombasa.
Spika wa bunge hilo la Mombasa Aharub Khatri amewarai wajumbe wa bunge hilo, kuendeleza harakati zao kwa njia mwafaka na kuambatana na sharia ili kuhakikisha miswada muhimu iliyowasilishwa bungeni awali inajadiliwa na kupitishwa.
Spika Khatri amesema mswada wa huduma bora za afya, ule wa utoaji majina ya maeneo mbalimbali sawa na ule wa kuangazia mabadiliko ya tabianchi katika kaunti hiyo uliyowasilishwa bungeni itahakikisha inajadiliwa na kupitishwa.
Wakati uo huo, amewahimiza wajumbe hao kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ya kisheria katika kuangazia ukaguzi wa fedha na miradi mbalimbali inayoidhinishwa na serikali ya kaunti ya Mombasa.