Story by Rasi Mangale –
Bunge la kaunti ya Kwale limepitisha bajeti ya shilingi bilioni 9.8 ya makadirio ya matumizi ya serikali ya kaunti hiyo ya mwaka wa kifedha 2021/2022.
Akizungumza na Wanahabari nje ya majengo ya bunge hilo Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge hilo Chirema Kombo amesema shilingi bilioni 6.3 zitatumika kuendeleza shughuli za serikali huku shilingi bilioni 3.4 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Chirema amesema sekta ya elimu imenufaika na mgao mkubwa wa fedha katika bajeti hiyo kwa lengo la kuendeleza miradi ya elimu katika kaunti.
Kwa upande wake mjumbe wa wadi ya Mwereni katika bunge hilo Manza Beja, amesema ugavi wa fedha hizo katika wadi za kaunti hiyo umetekelezwa kwa usawa.