Story by Mwanaamina Fakii-
Bunge la kaunti ya Kwale limepiga kura kwa kauli moja mswada wa kutokuwa na imani na Waziri wa maswala ya vijana, jamii na ukuzaji talanta katika serikali ya kaunti ya Kwale Ramadhan Bungale na kumtimua mamlakani.
Mswada huo ambao uliwasilishwa bungeni humo na Mwakilishi wa wadi ya Ramisi Raia Mkungu na kuungwa mkono na Mwakilishi wa wadi ya Puma James Dawa umepigiwa kura 20 dhidi ya kura 8 na kumtimua mamlaka Waziri Bungale.
Akizungumza na Wanahabari katika majengo ya bunge hilo, Mwakilishi wa wadi ya Ramisi Raia Mkungu amesema bunge hilo limechukua hatua hiyo kutokana na ripoti ya mhasibu mkuu wa fedha za umma kwamba Bungale alihusika katika sakata ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati alipokuwa Afisa mkuu katika Wizara ya Biashara na maendeleo mwaka wa 2018.
Kwa upande wake Mwakilishi wa wadi ya Kasemeni Anthony Yama amesema juhudi zao za kuutetea mswada huo ili kuzuia kutimuliwa mamlakani Bungale hazifaulu kutokana na idadi ya kura zilizopigwa.
Hata hivyo bunge hilo limetuea wajumbe 7 kuchanguza madai yanayomkabili Bungale na kuwasilisha ripoti yao bungeni humo katika muda wa wiki moja na ikiwezekana Bungale pia anaweza kufika mbele ya bungeni hilo ili kujitetea.
Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu usalama imezuru kaunti ya Mombasa kujadili mageuzi ya sheria ya kudhibiti bidhaa mbalimbali zinazoingizwa humu nchini.