Bunge la kaunti ya Kwale linatarajiwa kusitisha shughuli zake kuanzia hapo kesho kufuatia tishio la maambukizi ya virusi va Corona.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge la kaunti ya Kwale kuhusu afya Mwinyi Mwasera amesema shughuli za bunge hilo zitasitishwa kwa muda wa siku 15 kwa kuzingatia agizo lililotolewa na serikali la kusitishwa kwa makongamano.
Mwasera vile vile amesema kuwa wameeka mikakati hitajika ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya kaunti hio.