Aliyekuwa mwenyekiti wa hazina ya maendeleo ya vijana Bruce Odhiambo ameaga dunia.
Odhiambo amefariki mapema leo katika Hospitali ya Nairobi, alikolazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi, baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa mda mrefu.
Mwezi wa Oktoba mwaka jana, marehemu Odhiambo alienda India kutafuta matibabu, baada ya kuhisi mpigo wa moyo usio wa kawaida.
Alirudi humu nchini mwezi wa Novemba, lakini hali yake ya kiafya ikazidi kuzorota, na baadaye kulazwa katika hospitali ya Nairobi.
Kifo cha Bruce ni pigo k ubwa kwa tasnia ya mziki ikikumbukwa kuwa aliwahi kuwa mwazilishi wa kundi la Safari Sound Band na pia mmiliki wa studio ya Johari Cleff.