Picha kwa hisani –
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva TID amezungumzia uhusiano wa Harmonize na Kajala Fridah na kumshauri Harmonize kuwa anatakiwa atulie hapo hapo kwani Kajala ni mwanamke anayejituma sana.
Pia ameeleza kuwa wawili hao wakiachana basi atadiriki kugombana na Harmonize.
Mbali na hilo TID ametoa sababu za kutokufanya show zake Dar es Salaam na kusema unaweza kutumia nguvu wakaja watu kumi kwenye show watu wengi wana wivu sana.