Story by Hussein Mdune & Rasi –
Bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama cha UDA imewaahidi wanachama wake kwamba zoezi la kura ya mchujo wa chama hicho litaandaliwa kwa njia huru na haki.
Akizungumza katika Kongamano lilowaleta pamoja wagombea wa nyadhfa mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho katika ukumbi wa kitamaduni mjini Kwale, Katibu mkuu wa Bodi hiyo Victor Welden amesema hakuna mgombea atakayepewa tiketi ya moja kwa moja.
Welden amesema zoezi hilo la kura za mchujo wa wagombea wa chama cha UDA litaanza rasmi tarehe 9-16 mwezi Aprili mwaka huu huku akiwataka viongozi kuwasajili wanachma wengi ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikishwa kwa njia ya haki na uwazi.
Kauli yake imeungwa mkono na Mwanachama cha Bodi hiyo Chacha Matiko aliyewataka viongozi kudumisha amani wakati wa kura hizo za mchujo huku akiwataka viongozi wa chama hicho kushirikiana vyema.