Wahudumu wa bodaboda mjini Kwale, watavuna kutokana na msako wa magari ya uchukuzi unaoendelezwa na maafisa wa usalama kote nchini, usafiri wao ukisalia wa kipekee mjini humo.
Wahudumu hao wameahidi kuwabeba abiria hadi maeneo yao ya kazi, kwa sharti kuwa walipe nauli bila kulalamika.
Abiria wanaoelekea Kombani watalipishwa kati ya shilingi mia tatu na mia nne kupitia usafiri wa bodaboda.
Aidha wasafiri wanaoelekea maeneo ya Likoni na Lungalunga watagharamika zaidi , wahudumu wa boda boda wakiwatoza shilingi mia 6 na mia 8 mtawalia.
Wasafiri wengi kote nchini wamekwama kwa kukosa usafiri baada ya wahudumu wa magari kuficha magari yao baada ya sheria za trafiki maarufu za michuki kuanza kutumika tena leo.
Taarifa na Michael Otieno