Story by Hussein Mdune –
Katika juhudi za kuimarisha wakulima wadogo wadogo kupitia Bima inayosimamia maswala ya mimiea ya PULA na IPA imeanza zoezi la kuwalipa fidia wakulima 13,533 ambao waliathirika na kiangazi mwaka uliopita.
Kulingana na Afisa mkuu mtendaji wa Bima inayosimamia maswala ya mimiea ya PULA, Rose Goslinga, tayari Bima hiyo imetenga shilingi milioni 85 za kuwalipa fidia wakulima hao ambapo kila mkulima atapata zaidi ya elfu sita.
Akizungumza katika bustani ya baraza park mjini Kwale Goslinga ameweka wazi kwamba wakulima hao ambao wanajihusisha na kilimo cha mimiea ya aina mbalimbali kama vile Mahindi, Mawele, Pojo miongoni mwa mimea mingine kwamba fedha hizo zitawasaidia kuimarisha shughuli zao za kilimo.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo na ufugaji katika serikali ya kaunti ya Kwale Joan Nyamaso amesema shilingi milioni 13 zitafidiwa wakulima 2,954 kutoka kaunti ya Kwale ambao mimea yao iliathirika na kiangazi.