Shilingi bilioni 1.2 zimetengwa kwa ajili yakuujenga upya uwanja wa kaunti ya Mombasa.
Uwanja huo kwa sasa umebakia kuwa mahame licha ya kuwepo katika ahadi ya viwanja vitano iliyowekwa na serikali wakati wa kampeni ya mwaka 2017.
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amewahakikishia wanamichezo kuwa uwanja huo wenye historia ndefu utajengwa na kufikia hadhi ya kimataifa.
Vilevile amezidi kutofautiana na wapinzani wake wanaozidi kumkosoa kuhusiana na kutokarabatiwa kwa uwanja huo akisema awamu yake ya kwanza kama gavana ilikua ngumu.
Uwanja wa kaunti ya Mombasa umekua mahame kwa siku nyingi na kumekua na vilio kutoka kwa washikadau wamichezo lakini sasa nuru imeonekana na gavana Joho anasema uwanja huo utapanuliwa kuweza kukidhi mashabiki kati ya elfu kumi hadi kumi na tano.
Taarifa na Dominick Mwambui.