Picha kwa hisani –
Idara ya usalama imeteketeza badhaa ghushi zenye thamani ya shilingi milioni 24 katika eneo la Kibarani Kaunti ya Mombasa.
Akizungumza jana jioni baada ya kuongoza zoezi hilo,mshirikishi mkuu wa utawala Kanda ya Pwani John Elungata amesema bidhaa hizo ni vyakula vikiwemo mchele, unga wa ngano, mafuta ya kupikia na vyombo vya nyumbani.
Kulingana na Elungata, japo baadhi ya Wafanyibiashara huingiza bidhaa hizo ghushi pasipo na ufahamu, serikali imejitokeza kuwahamasisha ili kuhakikisha bidhaa bandia haziingizwi tena humu nchini.
Elungata amekanusha madai kwamba kuingizwa bidhaa gushi kumechangiwa na utepetevu wa Maafisa wa usalama na ufisadi miongoni mwa Maafisa wa mamlaka ya ushuru mipakani na hasa katika bandari ya Mombasa.