Picha kwa Hisani –
Aliyekuwa balozi wakenya nchini zambia Bi Sophy Kadzo Kombe amewashauri wazazi katika eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi kuwalinda watoto wao inavyostahili ili kuwaepusha na maovu.
Akizungumza katika eneo la Vishakani Bi Kadzo amesema kuwa wazazi wengi eneo hilo wameachia mashirika ya kijamii jukumu la kuwaelekeza watoto katika njia njema.
Hata hivyo ameitaka jamii kuwahusisha vijana na shughuli mbali mbali ili kuwaepusha na fikra potovu zinazowasukuma katika maovu.