Picha kwa hisani –
Mwakilishi wa kike kaunti ya Tana-river Bi Rehema Hassan amesema kuna haja ya bunge la kaunti hio kubuni sheria itakayoangazia masuala ya ufugaji ndani ya kaunti hio.
Akizungumza katika kaunti hio Bi Hassan amesema sheria hio itasaidia kuthibiti migogoro ya mara kwa mara kati ya jamii za wafugaji ambayo mara nyingi uchangiwa na suala la malisho ya mifugo hio.
Bi Hassan aidha amewakosoa wafugaji kutoka kaunti zengine wanaopenya katika kaunti ya Tana-river na kulisha mifugo yao katika mashamba ya wenyeji,akisema hatua hio imechangia mapigano.
Bi Hassan amewataka maafisa tawala kushirikiana na idara ya mifugo kuidhinisha sheria zitakazozuia mizozo kati ya wakulima na wafugaji.