Mbunge was Likoni Mishi Mboko ameonyesha kutoridhishwa na hatua ya baadhi ya viongozi kudaiwa kupokea hongo ili kuitupilia mbali ripoti ya sakata ya sukari gushi iliyowasilishwa bungeni kujadiliwa.
Bi Mboko ameitaja hatua hiyo kama njia inayodhihirisha wazi kuwa kuna baadhi ya viongozi wanahusika kwenye sakata za ufisadi humu nchini.
Ameitaja ripoti hiyo kama iliyokuwa na mambo muhimu ya kujadiliwa na kupeana mwafaka lakini hatua iliyochukuliwa na baadhi ya wabunge huenda ikalemaza juhudi za kupiga vita ufisadi humu nchini.
Amesema ripoti hiyo ilikuwa ina malenga ya kuibuka na njia mwafaka za kudhibiti uingizaji wa Sukari Bandia humu nchini lakini jinsi ilivyokuwa bungeni ni jambo la kushangaza.
Taarifa na Hussein Mdune.