Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko ameitaka serikali kuu kuwafidia kwa wakati wakaazi wa eneo la Likoni watakaothirika na mradi wa barabara wa Dongo Kundu.
Bi Mboko amesema kuwa fidia hio itawasaidia wakaazi hususan vijana kuidhinisha miradi ya kiuchumi na kujikimu kimaisha.
Mbunge huyo wa Likoni amesema kuwa viongozi wa eneo hilo watafanya juhudi kuhakikisha wakaazi watakaoathirika na mradi huo wanapata haki yao.
Taarifa na Hussein Mdune.