Picha kwa hisani –
Mimba za utotoni zimeripotiwa kuongezeka katika kaunti ndogo ya Likoni hasa eneo la Mtongwe tangu janga la Corona kushuhudiwa nchini.
Mwalimu na mfanyibiashara wa soko la Sokomjinga huko Mtongwe Bi Lydia Kwamboka, amelitaja janga la Corona kama chanzo cha visa hivyo miongoni mwa wasichana wadogo kufuatia kukosa mahitaji muhimu kwa wazazi wao.
Kulingana na Kwamboka, wasichana wengi hushawishika na vijana hususan wanaohudumu bodaboda ili kupata pesa za kununua sodo.
Wakati uo huo amemtaka mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko, kuweka mikakati ya kudumu kuhusu maisha ya mtoto wa kike hasa kipindi hiki cha janga la Corona.