Story by Our Correspondents –
Mama wa taifa Bi Margaret Kenyatta amewahimiza wataalam wa kiafya nchini kuhakikisha wanaibuka na huduma maalum za kukabiliana na makali za maradhi yasioweza kutibiwa ikiwemo ugonjwa wa Saratani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sera ya kwanza ya huduma maalum ya kupunguza makali ya maradhi yasioweza kutibiwa katika halfa iliyoandaliwa jijini Nairobi, Mama wa taifa amesema mpango wa afya kwa wote unafaa kupiga jeki zaidi.
Bi Kenyatta akidokeza kuwa huduma hiyo humpa matumaini makubwa mgonjwa wakati anapougua huku akidai kwamba kuboreshwa kwa huduma za afya nchini kutapunguza gharama za maradhi mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu mkuu msimamazi katika Wizara ya Afya nchini Dkt Mercy Mwangangi amesema sera hiyo mpya itasaidia serikali kutekeleza mpango wa kuboresha zaidi vituo vya afya nchini.