Picha kwa hisani –
Naibu gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amemkosoa gavana wa Mombasa Hassan Joho, kwa kuingilia shughuli za kaunti hiyo katika kampeni zake za siasa.
Achani ameitaja hatua ya Joho kuwa inayolenga kumdhalilisha gavana wa Kwale Salim Mvurya, katika masuala ya maendeleo.
Naibu huyo wa gavana amemtaka Joho kukoma kumdhalilisha Mvurya katika mikutano ya kisiasa ya kumpigia debe mgombea wa chama cha ODM Omar Boga.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya, amewakosoa vikali wale wanaoendeleza siasa za matusi dhidi ya Achani.
Mvurya amesema hatua ya kumuunga mkono Achani katika azma yake ya kuwania ugavana wa Kwale mwaka wa 2022 haijawafurahisha wapinzano wao.
Viongozi hao walikuwa wakizungumza huko Msambweni katika mkutano wa kumpigia debe mgombea huru Feisal Bader.