Story by Our Correspondents –
Naibu Gavana wa Kwale Bi Fatuma Achani aliyetangaza azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022, amemtaja Chirema Kombo kama mgombea mwenza wa uchaguzi huo.
Bi Achani amesema baada ya kikao cha mazungumzo kwa mda mrefu na viongozi kutoka eneo la Lungalunga, Matuga, Msambweni na Kinango, amefikia hatua ya kumtaja Chirema ambaye ni mjumbe wa wadi ya Samburu/Chengoni kama mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande Chirema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Kwale, amepongeza hatua hiyo akidai imeonyesha imani ya uwajibikaji katika kuongozi huku akiahidi kufanikisha ajenda za maendeleo.
Hata hivyo kiti cha ugavana wa Kwale kimewavutia wanasiasa wengi akiwemo Balozi Chirau Ali Mwakwere, Mwanasiasa Lung’anzi Chai, Bi Fatuma Achani miongoni mwa viongozi wengine.