Benki kuu ya Kenya imezindua rasmi sarafu mpya itakayotumika humu nchini kuanzia hii leo.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa kuzinduliwa kwa sarafu hio sio tu kubadilisha thamani ya sarafu ya humu nchini bali kuwasilisha tamaduni na historia ya taifa kwa njia ya kipekee.
Rais amesema kuwa kuzinduliwa kwa sarafu hiyo yenye vigezo maalum vya kuwawezesha watu wenye ulemavu wa macho kuitambua ,kumeambata na katiba ya nchini.
Kwa upande wake gavana wa benki kuu ya Kenya Patrick Njoroge amesema kuwa sarafu hiyo tayari ni halali kutumika kwani imechapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali.
Kinyume na sarafu zinazotumika kwa sasa nchini zenye picha za marais waliostaafu Daniel Arap Moi na Jomo Kenyatta, sarafu hio mpya itakua na picha za vitu vinavyoashiria taifa la Kenya.
Taarifa na Radio Kaya.