Picha kwa hisani –
Mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya amewataka wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Kilifi kutokubali kuhadaiwa na ruzuku ya kununua magari ya shilingi milioni mbili ili kupitisha mswada wa BBI.
Kulingana na Baya, viongozi wote wa kaunti ya Kilifi hawaungi mkono mchakato wa BBI, lakini wajumbe hao wataupitisha mswada huo kutokana na tamaa zao za kifedha.
Amesema siasa za kukishabikia chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, zimefika kikomo na wakaazi wa Kilifi hawatakubali kuhadaiwa tena.