Kenya itapiga hatua kimaendeleo, uiano na demokrasia iwapo itaandaa kura ya maamuzi kuhusu ripoti ya jopokazi la maridhiano BBI.
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameitaja ripoti hiyo kama mwafaka na itakayobadili mfumo wa uongozi na ujamii humu nchini.
Nassir amewakosoa vikali baadhi ya Viongozi wa kisiasa wanaoipinga ripoti hiyo bila ya kufahamu vipengele muhimu vilivyo ndani ya ripoti hiyo.
Wakati uo huo, Mwakilishi wa kike Kaunti ya Mombasa Bi Asha Hussein amewarai Wakaazi wa Kaunti ya Mombasa kuisoma ripoti hiyo na kufanya maamuzi ya busara pindi kura ya maoni itakapoandaliwa nchini.