Picha kwa hisani –
Wadau wa sekta ya Utalii katika kaunti ya Kilifi, wanadai kuwa kufanikishwa kwa mchakato wa BBI kutaleta mabadiliko makubwa katika sekta hiyo.
Kulingana na Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa hoteli kaunti ya Kilifi Maureen Awour, mchakato wa BBI utasitisha mvutano unaoshuhudiwa kila baada ya uchaguzi ambao huchangia sekta hiyo kudidimia.
Akuzungumza na Wanahabari mjini Malindi, Maureen amesema ufisadi pia utapata suluhu kwani umechangia wawekezaji wangi kutoroka humu nchini kutokana na mazingira duni ya uwekezaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wamiliki wa mikahawa, vilabu na maeneo ya burudani kaunti ya Kilifi Eric Mwashigadi amesisitiza haja ya wanasiasa kuzingatia ndihamu wakati wa kuhamasisha umma kuhusu mchakato huo.