Picha kwa hisani –
Baraza la mashauri ya Kiislamu nchini KEMNAC linaahidi kuunga mkono kikamilifu mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba BBI kutokana na agenda za msingi za kupigania amani katika taifa hili.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema mchakato huo ni ukurasa mpya katika taifa hili, akiwarai wakaazi wa eneo la Pwani kuiunga mkono kikamilifu.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sheikh Ngao amesema BBI ina vipengele msingi vinavyomhusu Mkenya moja kwa moja mashinani huku akihoji kuwa vipengele hivyo iwapo vitatekelezwa kikamilifu basi taifa hili litapiga hatua katika maswala ya mshikamano.
Wakati uo huo, amezikosoa siasa za mabishano zinazoendelezwa katika kuhusu mchakato huo, akiwataka wanasiasa nchini kuhubiri amani pasipo na malumbano.