Picha kwa Hisani –
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amewakosoa vikali wanasiasa na wakenya wanaoupinga mchakato wa kuwaunganisha Wakenya wa BBI, akisema hawana nia njema kwa taifa hili.
Raila aliyeonekana kuelekeza kauli yake kwa Naibu Dkt Rais William Ruto, amesema mchakato wa BBI ni muhimu kwa wakenya kwani unalenga kubadili mwelekeo wa taifa hili katika miaka ijayo.
Raila aliyekuwa akizungumza katika mkutano wa wajumbe wa chama cha ODM katika hoteli ya ‘Wild waters’ kule Mombasa, amesema ni kupitia mchakato wa BBI ndipo taifa hili litashuhudia maendeleo hadi mashinani.
Wakati uo huo amewataka Wakenya kutohadaiwa na baadhi ya watu wachache wasio na malengo ya maendeleo ya taifa hili, huku akisisitiza kuwa mchakato wa BBI utampungua gharama ya maisha mwananchi.