Picha kwa hisani –
Bunge la kaunti ya Trans-Nzoia linatarajiwa kuupigia kura mswada wa BBI mwendo wa saa nane mchana hii leo.
Akizungumzia suala hilo kiongozi wa waliowengi katika bunge hilo Patrick Kisiero amesema mswada huo una umuhimu kwa wananchi ikizingatiwa kwamba utaongeza mgao wa rasilimali katika kaunti.
Kisiero amesema wakati wa vikao vya kukusanya maoni ya wakaazi wa kaunti hio kuhusu BBI vilivyoandaliwa juma lililopita,asilimia 80 ya wakaazi wa kaunti hio waliunga mkono ripoti hio ya BBI.
Kisiero amesema tayari amewashawishi wajumbe katika bunge hilo kuhakikisha wanaunga mkono ripoti hio.