Picha kwa hisani –
Katibu katika wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho amesema mchakato wa BBI hauna uhusiano wowote na azma ya kinara wa ODM Raila Odinga ya kuwania urais wa taifa hili kama inavyodaiwa.
Akihutubia wakaazi wa mlima Kenya Kibicho amewataka wakaazi wa eneo hilo kuunga mkono BBI ili wanafaike na nyongeza ya mgao wa rasilimali na kuchochea maendeleo ya eneo hilo badala ya kuhusisha ripoti hio na uongozi wa Odinga.
Kibicho amesema mabadiliko ya katiba kupitia kuidhinishwa kwa ripoti ya BBI yatapelekea eneo hilo la mlima kenya na maeneo mengine yanayopata mgao mchache wa rasilimali kutoka kwa serikali kupata nyongeza ya mgao huo.
Kauli ya kibicho inajiri huku mabunge saba ya kauntia yakiwa tayari yameupitisha mswada wa BBI baada ya kuujadili,bunge la kaunti ya Baringo likiwa la pekee kuuangusha mswada huo.