Msanii Bawazir amevunja kimya chake na kufichua kuwa atamchukulia hatua za kisheria kijana aliyemchafulia jina hivi majuzi.
Akilonga na Uhondo Bawazir aka City Boy amesema kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote kati yake na Bosco Makini aka Hommie Makini kama ilivyodaiwa hapo awali.
Bawazir akumbwa na kashfa ya kutumia vijana vibaya
Kulingana na Bawazir usemi wa kijana huyo ni kukosa kuelewa mambo na kujitafutia kiki.
Bawazir ameongeza kuwa watu wanapaswa kuheshimu jitihada anazofanya ili kujikuza kimziki na kibiashara badala ya kutafuta umaarufu kupitia njia chafu.
Taarifa na Dominick Mwambui.