Msanii Bawazir amekumbwa na kashafa kuwa halipi vijana anaowatumia katika kutangaza nguo anazouza katika duka lake.
Kashfa hiyo amelimbikiziwa na kijana kwa jina Bosco Makini maarufu kama Hommie Makini kutoka Malindi.
Akizungumza na meza yetu ya Uhondo, Hommie amesema kuwa waliingia katika mkataba na Bawazir lakini mkataba huo haukuheshimiwa.
Kulingana na Bosco ni kuwa baada ya kutangaza baadhi ya pamba katika duka la Bawazir angeachiwa baadhi ya pamba hizo, lakini hilo halikufanyika. Badala yake Bawazir alianza kumkwepa kila alipomtafuata ili atimize ahadi yake.
Hommie ameongezea kuwa meneja wa Bawazir alimpigia na kumwonya dhidi ya kumchafulia jina msanii wake. Jambo ambalo limezidi kumshangaza Hommie kwani anachotaka ni haki yake na meneja alikosa kuelewa mkataba waliokuwa nao na Bawazir.
Msikilize Hommie akielezea kisa hiki hapa.
Taarifa na Dominick Mwambui.
[…] Bawazir akumbwa na kashfa ya kutumia vijana vibaya […]