Kampuni Ya Uchimbaji Madini Ya Base Titanium katika kaunti ya Kwale imewafadhili kimasomo jumla Ya Wanafunzi 44 wa shule za upili Kutoka Jamii zisizojiweza eneo la Mwaweche, Kinondo.
Kulingana na afisa msimamizi wa miradi ya jamii katika kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium, Juma Lumumba ufadhili huo wa kima cha shilingi milioni 1.2 ni kati ya mikakati ya kampuni hiyo kuboresha uhusiano wake na jamii.
Kwa upande wake afisa wa elimu eneo la Msambweni Ahmed Mohamed amewataka wanafunzi waliopata ufadhili kutilia maanani masomo yao ili kubadili maisha yao siku za usoni.
Taarifa na Salim Mwakazi.