Picha kwa hisani –
Muungano wa wauguzi tawi la Taita Taveta umepuzilia mbali uamuzi wa serikali ya Kaunti hiyo wa kuwaachisha kazi kwa kushiriki mgomo.
Katibu wa muungano huo Reuben Matolo amesema zaidi ya wauguzi 500 wa kaunti hio wamekiri kupokea barua za kuachishwa kazi na serikali ya Kaunti hio.
Matolo amesema barua za kuachishwa kazi walizokabidhiwa wauguzi sio halali kwani serikali ya taita taveta haikufuata sheria hitajika za kuwaachisha kazi wahudumu hao wa afya.
Matolo ameikashifu serikali ya kaunti ya Taita Taveta kwa madai kwamba imeshindwa kushughulikia maslahi ya wahudumu wa afya wakiapa kutorejea kazini hadi kilio chao kitakapozingatiwa.