Picha kwa hisani –
Baraza la viongozi wa dini mbalimbali CICC limetaka mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba kupitia BBI umhusishe kikamilifu mwananchi mashinani na wala sio viongozi wa kisiasa pekee.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Muhdhar Khitamy amesema ni wazi shinikizo za BBI zinalenga kuwakimu Viongozi kisiasa na wala hazina malengo msingi kwa mkenya.
Kulingana na Khitamy, ni lazima viongozi wa kidini wasimame kidete na kukomesha ulafi huo wa mamlaka miongoni wa viongozi wa kisiasa nchini.
Hata hivyo, amezitaka taasisi zilizopewa majukumu ya kupigania haki, amani na usawa nchini kuwajibikia majukumu yao na wala sio kutumiwa na wanasiasa.