Story by Janet Shume-
Baraza la makanisa nchini NCCK limewahimiza wanasiasa kufanya kampeni za amani pasi na kutumia matusi wala vurugu ili taifa hili lishuhudie uchaguzi wa amani.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na viongozi wa makanisa mbalimbali kaunti ya Kwale, Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo kaunti ya Kwale Kasisi Nelson Mwanjala, amewahiza wanasiasa na wafuasi wao kukubali matokeo ya uchaguzi ili taifa liwe la amani.
Kiongozi huyo wa kidini vile vile amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kujitenga na semi za uchochezi ambazo huenda zikachangia vurugu za kisiasa.
Kwa upande wake Agnes Kitongaa ambaye ni Mwakilishi wa akina mama katika baraza hilo, amesema akina mama wamekuwa wakiathirika pakubwa baada ya uchaguzi kutokana na ahadi hewa ambazo hutolewa na wanasiasa.