Story by our Correspondents –
Baraza la magavana nchini limehairisha kongamano la 7 la ugatuzi lililokuwa limepangwa kuandaliwa katika kaunti ya Makueni kuanzia tarehe 23 hadi 26 mwezi Agosti.
Mwenyekiti wa baraza la hilo Martin Wambora amesema baraza la magavana limechukua hatua hiyo kutokana na taifa kuendelea kunakili idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona, likisema kuhairishwa kwa kongamano hilo kutadhibiti maambukizi zaidi.
Wambaro ambaye pia ni Gavana wa Embu amesema Baraza la Magavana litatoa tarehe rasmi ya Kongamano hilo baada ya kubaini kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini.
Wambora amesema baraza hilo limezingatia pia agizo la Rais Uhuru Kenyatta la kupiga marufuku mikutano ya umma, huku akiwahimiza wananchi kuzingatia masharti ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.