Picha kwa hisani –
Baraza la magavana limewataka wahudumu wa afya wanaoshiriki mgomo ikiwemo wauguzi na matabibu kurejea kazini na kwamba watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kuachishwa kazi.
Akizungumza wakati wa kikao magavana jijini Nairobi,mwenyekiti wa baraza hilo Wycliff Oparanya amesema wahudumu afya walioachishwa kazi baada ya kushiriki mgomo katika kaunti zao,hawatoajiriwi katika kaunti yeyote nchini.
Oparanya amesema baada ya sekta ya afya kugatuliwa serikali za kaunti zimejitahidi kuboresha sekta hio,akisema tangu mwaka 2017 kaunti zimetumia zaidi ya shilingi bilioni 5.2 kila mwaka kutimiza mahitaji ya wahudumu wa afya.
Kwa upande wake gavana wa Baringo ambae pia mwenyekiti wa kamati ya kukagua wafanyikazi katika baraza la magavana Stanley Kiptis amesema kwa sasa ni kaunti 13 pekee ambako wahudumu wa afya wanaendelea kutoa huduma kwa umma.