Story by Bakari Ali –
Baraza la mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC limeitaka Tume ya huduma za mahakama nchini JSC kusitisha zoezi la uteuzi wa makadhi watakaohudumu katika Mahakama zinazotatua mizozo ya jamii ya dini ya kiislamu.
Mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema zoezi hilo limekumbwa na utata mwingi na ni sharti tume hiyo inayoongozwa na Jaji mkuu nchini Martha Koome kusitisha zoezi hilo mara moja.
Sheikh Ngao amesema ni lazima zoezi hilo liendeshwe kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni zote za uteuzi wa makadhi nchini, akihoji kwamba jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa ni wazi kwamba kuna ufisadi.
Wakati uo huo, amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati swala hilo na kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa usawa na uwazi ili Mahakama za kadhi nchini ziwajikie majukumu yake kwa uwazi.