Story by Gabriel Mwaganjoni –
Baraza la mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC linaitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kulitanzua swala la uchafu katika kaunti hiyo.
Baraza hilo likiongozwa na mwenyekiti wake Sheikh Juma Ngao limesema Serikali ya kaunti hiyo imeshindwa kulidhibiti swala sugu la mitaro ya maji taka huku maeneo mbalimbali hasa kisiwani Mombasa yakikumbwa na uvundo mkali kufuatia kufurika kwa mitaro ya maji taka.
Akizungumza katika kaunti hiyo Sheikh Ngao amesema ni sharti swala hilo lidhibitiwe kwani limeshusha pakubwa hadhi ya kitalii ya jiji la Mombasa.
Kauli ya Ngao inajiri huku maafisa wa kituo cha polisi cha Central wakilazimika kuihama afisi yao mpya baada ya maji taka kufurika kituoni humo.