Picha kwa hisani –
Baraza la Mashauri ya Kiislamu nchini KEMNAC limezindua kampeni ya kuipigia debe mchakato wa BBI kote nchini.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema kampeni hiyo inayajumuisha mashirika mbalimbali ya Kiislamu nchini ili kufanikisha swala hilo la BBI.
Kulingana na Ngao, tayari mipangilio imewekezwa, na Baraza hilo kuzuru mashinani katika kila pembe ya nchi ili kuwafahamisha wakenya kuhusu umuhimu wa mchakato wa BBI.
Wakati uo huo amesema BBI itawanufaisha Waislamu kwa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia swala msingi la umoja na uiano.