Story by Ali Chete –
Mwenyekiti wa baraza la Mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC Sheikh Juma Ngao, amesema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana ndio chanzo kikuu cha vijana wa Pwani kujiunga na makundi ya kihalifu.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sheikh Ngao amesema swala hilo la ukosefu wa ajira na idadi kubwa ya Pwani kuishi kama maskwota kuchangia eneo hili kushuhudia idadi ya vijana kusajiliwa katika makundi ya kigaidi.
Kiongozi huyo wa kidini ameitaka serikali kuu kuliangazia swala la ajira kwa wakaazi wa pwani ili kudhibiti makundi ya kihalifu na ugaidi.