Picha kwa Hisani –
Viongozi wa dini mbali mbali nchini wamefanya kikao jijini Nairobi hii leo ili kujadili mipangilio ya jinsi ibada zitakavyoendelezwa.
Mwenyekiti wa baraza la dini mbali mbali linalotathmini ufunguzi wa nyumba za ibada askofu Antony Muheria ametaka hafla za mazishi kuendelezwa kama makongamano ya ibada na badala ya kuandaliwa kama vikao vya kijamii.
Muheria amesema kenya bado iko katika hatari ya maambukizi ya corona na kwamba viongozi wa kidini wanafaa kuendelea kuzingatia maagizo ya kuzuia maambukizi katika nyumba za ibada.
Askofu Muheria vile vile amewasihi wanasiasa kusitisha mikutano ya kisiasa kwani inaandaliwa kwa kukiuka masharti ya kiafya yaliowekwa na serikali na kuwaeka wakenya katika hatari ya maambukizi.