Mwanamziki wa mitindo ya ragga na R n B kutoka eneo la Malindi, Kaunti ya Kilifi, Mnyamwezi, afichua kuwepo kwa mipango ya kufanya kazi na msanii wa bongo flavaz kutoka Tanzania, Barakah the Prince. Msanii huyo amethibitisha haya kupitia njia ya simu na Radio Kaya.
Kulingana na Mnyamwezi, Barakah alipenda kazi yake alipokuwa ana cut and raise kwenye show ya Mauzo classic iliyojumulisha performances za Colonel Mustapha, Brown Mauzo na Barakah the prince ambayo ilifanyika Manyatta eneo la Diani, Kaunti ya Kwale mkesho wa kuvuka mwaka.
Kupitia kwa njia ya mahojiano ya simu, Mwanamziki huyo kutoka Tanzania alidokeza kuwa ana imani kubwa sana na msanii huyo na kuwa angemtaka Mnyamwezi kwenda Tanzania kwa gharama yake ili kufanya kazi naye.
Hii ni baada ya Barakah the prince kutangaza kuregea kwenye sanaa ya muziki baada ya kukaa kimya kwa muda sasa, na kutoa ngoma yake mpya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Machi 14,2020 iliyojulikana kama “Nimekoma”
Aidha sasa mashabiki wa wasanii hao wanangoja kazi hiyo mpya inayotarajiwa kufanywa hivi karibuni baada ya shirika la afya duniani WHO, kuweza kulidhibiti janga linalotukumba ulimwenguni la virusi vya korona (COVID-19)