Wakaazi wa Bamba kaunti ya Kilifi wamepata afueni baada ya barabara ya kutoka Mariakani hadi Bamba kuanza kutoa huduma kwa wakaazi hao.
Wakiongozwa na Kiongozi wa jamii ya eneo hilo la Bamba Emmanuel Nzai wamesema kukamilika kwa barabara hiyo ya umbali wa kilo mita 45 kwa kiwango kikubwa utalifungua eneo hilo kiuchumi.
Akizungumza huko Bamba, Nzai amesema mradi huo umewasaidia pakubwa wakaazi wa eneo hilo na utawawezesha kujihusisha na maswala ya biashara, na shughuli nyinginezo za kiuchumi ili kujiendeleza kimaisha.
Kwa upande wao wakaazi wa eneo hilo wakiwemo wahudumu wa magari, wametaja mahangaiko waliyoyapitia miaka 55 wakisubiri kujengewa kwa barabara hiyo iliyowachukua siku mbili kabla ya kufika mjini Mariakani.
Barabara hiyo imegharimu kima cha shilingi bilioni 2.2 kukamilika na inaunganisha eneo la Bamba na mjini Mariakani katika kaunti ya Kilifi.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.