Klabu ya Bandari imefuzu kwa nusu fainali ya mchuano wa Sport Pesa Super Cup kwa kuilza klabu ya Singida FC kwa ushindi wa 1-0.
Bandari wamepata ushindi huo kupitia njia ya penanti. Penanti hiyo imesukumwa kimnyani na mchezaji William Wadri.
Kwa sasa klabu ya Bandari inasubiri kucheza na mshindi kati ya AFC Leopards ya Kenya na Simba SC ya Tanzania.
Kama mchezaji bora wa mechi hiyo Wadri amepokezwa hundi ya dola za kimarekani 500 hii ni sawa na Ksh 50, 000.