Klabu ya Bandari imeandikisha ushindi 3-1 dhidi ya Posta Rangers katika mechi ya ligi kuu ncini iliyochezwa uga wa Camp Toyoyo, Jumamosi.
Bandari walichukua uongozi wa mechi kupitia kwa mchezaji Yema Mwana aliyepokea pasi safi kutoka kwa Lugogo katika dakika ya saba ya mchezo.
Katika dakika ya 23 Shaban Kenga kwa njia ya kichwa akawapa Bandari la pili katika dakika ya 23.
Calvin Odongo aliwapa Posta Rangers la kufutia macho kunako dakika ya 43 lakini katika kipindi cha pili Bandari walikuwa wakali zaidi na kuongeza bao la tatu kupitia kwa Wycliff Ochomo.
Taarifa na Dominick Mwambui.