Klabu ya Bandari imeendeleza msururu wa ushindi kwa kuilaza Tusker Fc 1-0 kwenye mechi kali iliyochezwa katika uga wa Ruaraka Jijini Nairobi.
Bandari wamepata bao la ushindi kupitia Yema Mwana katika dakika ya nne ya mchezo.
Na ushindi huu Bandari wanashikilia nafasi ya pili katika msiamamo wa ligi kuu nchini KPL wakiwa na pointi 48.
Ushindi huu ulikuwa wa kulipiza kisasi kwani katika mkondo wa kwanza wa msimu huu Bandari walitandikwa mabao 2-0 na Tusker nyumbani.
Katika matokeo mengine ya ligi kuu.
Thika United 1-1 Wazito
Ulinzi Stars 0-1 Sony Sugar
Sofapaka 0-1 Vihiga United
Nakumatt 1-3 AFC Leopards
Mathare United 1-1 Kariobangi Sharks
Taarifa na Dominick Mwambui.